Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, mamia ya waumini katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, hususan Tanzania na Kenya, wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika majlisi za Muharram zinazofanyika katika misikiti, husainiya na vituo vya dini kwa ajili ya kuhuisha tukio la Ashura na kutafakari ujumbe wa milele wa Karbala.
Mikoa na miji mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Bukoba, Tabora, Tanga, Moshi pamoja na maeneo mengine mengi, imeshuhudia mikusanyiko mikubwa ya waombolezaji wanaokusanyika kila siku kusikiliza mawaidha, khutba na historia ya harakati ya Imam Hussein (as) dhidi ya dhulma na upotovu.

Maombolezo ya Imam Hussein (as) Katika Hawza ya Bibi Zainab (as) Kirigiti Kenya
Katika majlisi hizo, wahadhiri na wahutubu wamewasilisha mada mbalimbali zinazohusu sababu za mapinduzi ya Imam Hussein (as), masaibu yaliyomkuta yeye na Ahlul-Bayt wake huko Karbala, pamoja na athari za tukio hilo katika kuhuisha maadili ya Kiislamu na kulinda misingi ya dini.

Maombolezo ya Imam Hussein (as) Katika Hawza Imam Swaadiq (as) Jijini Dar-es-alam Tanzania
Aidha, wahutubu wamewakumbusha waumini kuwa harakati ya Imam Hussein (as) ilikuwa ni harakati ya kutetea haki, uadilifu na mafundisho sahihi ya Uislamu, huku wakisisitiza umuhimu wa kushikamana na dini, kupinga dhulma na kuendeleza maadili aliyoyatetea kwa kujitoa muhanga.

Maombolezo ya Imam Hussein (as) Katika Hawza ya Khatamul Anbiya, Arusha Tanzania
Washiriki wa majlisi hizo wameeleza kuwa kuadhimisha kumbukumbu ya Karbala ni njia ya kuendeleza ujumbe wa Imam Hussein (as) katika vizazi vya sasa na vijavyo, huku wakiahidi kuendelea kushikamana na misingi ya haki, uhuru na uadilifu ambayo ndiyo kiini cha harakati yake tukufu.

Maombolezo ya Imam Hussein (as) Katika Msikiti wa Ahlulbayt (as) Moshi Tanzania
Majlisi za Muharram zinaendelea katika maeneo mbalimbali ya Afrika Mashariki katika mazingira ya huzuni, mapenzi kwa Ahlul-Bayt (as) na hamasa ya kuhuisha ujumbe wa Ashura, ambao umeendelea kuwa nuru ya uongofu na chachu ya mapambano dhidi ya dhulma katika kila zama.

Maombolezo ya Imam Hussein (as) Katika Huseiniya ya Imam Ridhwa (as) Arusha Tanzania

Maombolezo ya Imam Hussein (as) Katika Msikiti wa Zainabiya Bukoba
Maoni yako